Kaunti ya Migori inajiandaa kuandaa tamasha la tano la Piny Luo litakaloadhimu utamaduni wa Waluo, urithi wao, utambulisho, desturi na mienendo yao.

Akizungumza na wanahabari, Katibu wa Kaunti ya Migori alisema tamasha hilo litafanyika kwenye uwanja wa michezo wa Migori.

Tamasha hilo litajumuisha ngoma za asili, vyakula vya kitamaduni, na maonyesho ya mavazi.

Chanzo: Ofisi ya Katibu wa Kaunti



